Tangu mahakama ya Kenya ilipotoa hukumu kwa raia wawili wa Iran kwenda jela kifungo cha maisha kutokana na mashtaka yanayohusiana na ugaidi
mapema mwezi huu, hali ya baadaye ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya
Nairobi na Tehran imekuwa wa mashaka, kukiwa na uwezekano wa kurudisha
nyuma matumaini ya Iran ya kupanua shughuli na uwepo wake kisiasa nchini
Kenya kwa miaka ijayo.
Sayed Mansour (katikati) na Ahmad Mohammed (kulia), wote wawili ambao ni raia wa Iran, wanafungwa pingu mara tu baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela hapo tarehe 6 Mei kutokana na mashtaka yanayohusiana na ugaidi, ikiwa ni pamoja na kumiliki iliyodaiwa kuwa milipuko kwa ajili ya kutumia katika mashambulio ya bomu. [Simon Maina/AFP]
Mgogoro huo wa kidiplomaisa ulitokana na shambulio la ugaidi
lililoteguliwa nchini Kenya ambalo lililotolewa hukumu na mahakama
ambalo lilikuwa limepangwa na Ahmed Mohammed, mwenye umri wa miaka 50, na Sayed Mansour, mwenye umri wa miaka 51, wote wawili raia wa Iran.
Wanaume hao wawili walikamatwa mwezi Juni mwaka uliopita nje ya Laico
Regency, hoteli yenye nyota tano inayomilikiwa na Mlibiya katikati ya
Nairobi, siku nane baada uchunguzi mkubwa uliofanywa na Kitengo cha
Polisi Kinachopambana na Ugaidi.
Tarehe 2 Mei, walitiwa hatiani kwa kumiliki kilogramu 15 za milipuko
yenye nguvu ya RDX, ambayo polisi waligundua kufukiwa kwenye uwanja wa
gofu. Mahakama ya Nairobi ilisema Mohammed na Mansour walishukiwa kuhusika na ulipuaji bomu uliopangwa na mtandao wa kigaidi huko Mombasa na Nairobi. Wanaume wote hao wawili walikana mashtaka hayo.
Lakini polisi wa Kenya walitetea uamuzi wao wa kuwakamata na kuwafungulia mashtaka Wairani hao wawili.
Msemaji wa polisi Charles Owino aliiambia Sabahi kwamba polisi
hawakuwawekea wanaume hao, wala maofisa waliowakamata walifanya hivo
kutokana na maelekezo kutoka kwa serikali yoyote ya nje wakati
walipowafunga.
"Polisi wa Kenya walifanya uchunguzi wa kina kuhusu wanaume hao
wawili, hivyo kuzuia uhalifu mkubwa wa kigaidi kutokutokea katika nchi,"
Owino alisema. "Nina furaha kwamba tulitahadharishwa na kwamba mwishowe
tuliendesha mashtaka kwa mafanikio."
Baada ya Mohammed na Mansour kuhukumiwa kwenda jela maisha tarehe 6
Mei, vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa viliripoti kuwa
Wairani hao wawili walikuwa wakifanya kazi na kikosi maalum cha Quds,
kitengo cha siri cha kikundi cha Ulinzi cha Mapinduzi ya Kiislamu cha
Iran ambacho hufanya operesheni nje ya nchi.
Balozi wa Iran nchini Kenya Malik Hussein Givzad alikana madai hayo,
akisema wanaume hao wawili wa nchini kwake walikuwa watalii nchini Kenya
wakiwa na viza halali.
Kutoka siku ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Givzad aliiambaia gazeti la
Daily Nation la Kenya kwamba Iran ina uhusiano mzuri wa kibiashara na
Kenya na kwamba kutiwa hatiani kwa Mohammed na Mansour kusingesababisha
kuvunjwa kwa uhusiano wa kidiplomasia.
"Huu ni mchakato wa mahakama, ambao tunauheshimu," Givzad alisema,
akiongezea kwamba Iran itawasaidia wanaume hao wawili kukata rufaa dhidi
ya hukumu hiyo.
'Kenya inapaswa kutaka majibu'
Sio kila mmoja ana matarajio mazuri kuhusu kuhusu siku zijazo za uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Iran.
"Serikali ya rais Uhuru Kenyatta inapaswa kuwa jasiri na kukata
uhusiano huu wa hatari wa kidiplomasia na Tehran kama kutakuwa na
ushahidi wa kutosha kwamba Wairani waliokamatwa ni mawakala wa siri wa
Walinzi wa Jamhuri ya Iran, kama ambavyo Polisi wa Kuzuia Ugaidi na
Intelijensia ya Usalama wa Taifa wamekuwa wakidai," alisema Ignacious
Kamau Njoroge, ofisa usalama aliyestaafu, mwenye miaka 67 katika jeshi
la Kenya na mkurugenzi wa shirika la upelelezi la Global Eye Spies &
General Investigations iliyo na makao mjini Nairobi.
Njoroge alisema Kenya inapaswa kumrejesha balozi wake huko Iran na
kutuma barua ya malalamiko kwa serikali ya Iran na Umoja wa Mataifa kwa
sababu ya ukubwa wa tuhuma na majanga ambayo ingetokea iwapo mlipuko huo
ungefanyika.
"Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya inapaswa kuacha njia zake za sasa na
msimamo wa 'biashara kama kawaida' na kumuita kwa haraka balozi wa Iran
nchini Kenya na kumuagiza aelezee anachokijua kuhusu mashtaka ya pande
zote mbili badala ya balozi kutoa taarifa zisizoshawishi na kutoa
maelezo ya kukiri kosa katika mkutano na vyombo vya habari," Njoroge
aliiambia Sabahi.
"Na, sababu Wairani walioshitakiwa dhahiri walipinga kushirikiana na
waendesha mashtaka na wanaowahoji wa Kenya kama mwendesha mashtaka
alivyoeleza mahakamani, Kenya inapaswa kutaka majibu kutoka Iran,
vinginevyo tutahitimisha kwamba hawa wawili waliapa faragha na serikali
zao ili kubaki kimya kutunza utambulisho wao na matakwa ya nchi yao,"
alisema Njoroge.
Serikali ya Kenya inapaswa pia kutazama jinsi takriban kilogramu 15
za vifaa vya ulipuaji vilivyoingia nchini bila kutambulika, alisema
Njoroge.
"Serikali inapaswa kuchunguza kwa kina kutoka katika serikali ya Iran
jinsi nchi hizi mbili zilivyopata vifaa vya kutengenezea mabomu, hati
zao za utambulisho hasa ni zipi na ni wapi walikuwa wakilenga," alisema.
Kenya sio uwanja wa michezo kwa 'misheni za kulipiza kisasi za Iran'
Robert Kamau, mhadhiri wa uhusiano wa kimataifa na diplomasia katika
Chuo Kikuu cha Nairobi, alisema Kenyatta anapaswa kukamata fursa hii
wakati jumuiya ya kimataifa ikifuatilia.
"Rais Kenyatta, anayejaribu kushinda upendeleo wa jumuiya ya
kimataifa na ushirikiano baada ya mashtaka yake ya Mahakama ya Kimataifa
ya Makosa ya Jinai (ICC), anapaswa kukamata fursa sasa hivi na kutoa
ujumbe mkali kwamba Iran ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa
ulimwengu na kwamba Kenya inapaswa kutofumbia macho vitendo hivyo katika
himaya yake," aliiambia Sabahi. "Hii ndiyo sababu hasa [Kenya] ilijitolea wanajeshi wake na rasilimali kupigana na al-Shabaab kwa kina nchini Somalia."
"Nina uhakika kuwepo kwa Wairani na shughuli nchini Kenya zinakwenda
zaidi ya nyanja halali za kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni,"
alisema Kamau. "Kwa hakika Irani na shirika lake la usalama
wanashughulikia kwa siri ugaidi na uchochezi, ili kulipiza kisasi dhidi
ya serikali ya Israeli na Marekani, nchi hizo kuu mbili ambayo
inazichukia."
"Lakini Kenya, kama nchi inayopenda amani na inapaswa kuakataa kuwa
uwanja wa michezo kwa ajili ya misheni ya ulipizaji kisasi wa Iran nje
ya nchi," alisema.
Njoroge alisema mkutano unaofaa wa kipelelezi una uwezekano wa
kuonyesha kwamba shambulio lililokusudiwa kuhusu Kenya linaoana kwa
mtindo wa kiharamia wa Kiirani. Tarehe 13 Februari, 2012, walipuaji wa
Iran walimvamia mtumishi wa ubalozi wa Israeli katika mji mikuu ya India
na Georgia, na siku moja baadaye walipanga kufanya mashambulio kama
hayo huko Thailand na Azerbaijan lakini walikwamishwa. Kama sehemu ya
kiwango chao cha utaratibu wa kufanya kazi, serikali hiyo ilikanusha
vikali kuhusika na mashambulio hayo pia, alisema Njoroge.
Simiyu Werunga, ofisa jeshi mtaafu wa Kenya na Mkurugenzi mkuu wa
Kituo cha Afrika kwa ajili ya Usalama na Stadi za Kimkakati, alisema
hakuna yeyote aliyetarajia kwamba serikali ya Iran itajitokeza hadharani
na kukiri kutuma wakala wa ulipuaji bomu nchini Kenya.
"Kikosi cha Polisi cha Kenya [Kitengo] na wakala wa upelelezi wa
kitaifa, Shirika la Upelelezi la Taifa, vinapaswa kumpa taarifa rais
ipasavyo pamoja na taarifa sahihi za kipelelezi kuhusu uhusika wao
katika kesi hii ili mkuu wa nchi atoe agizo la uamuzi wa hatua za
kidiplomasia kuhusu upelelezi thabiti," Werunga alisema.
0 comments:
POST A COMMENT