Michezo ya Ligi Kuu Uingereza iliendelea Jumamosi ya January 23 kwa michezo kadhaa kupigwa, mchezo wa kwanza uliyochezwa wa Ligi Kuu Uingereza ni mchezo kati yaLiverpool dhidi ya Norwich City, ulipigwa mapema kabla ya michezo mingine kuchezwa.Liverpool wakiwa ugenini walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-4.
Baada ya hapo klabu ya Man United ambayo ilikuwa katika dimba lake la nyumbani Old Trafford, imekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Southampton, Man United ambao bado kocha wao Louis van Gaal yupo katika wakati mgumu wa kuokoa kibarua chake, walishindwa kusawazisha goli hilo, baada ya kufungwa dakika za lala salama.
Goli la Southampton lililofungwa dakika ya 87 ya mchezo na Charlie Austin limeifanyaMan United kuendelea kuwa nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi, huku ikiwa na point 37 katika michezo 23, Huu ni mchezo 6 wa Man United wanapoteza toka kuanza kwa msimu wa 2015/2016.
Matokeo ya mechi nyingine za Uingereza zilizochezwa Jnuary 23
0 comments:
POST A COMMENT