
Kocha mzawa ambae ameiongoza timu ya taifa kwa muda mrefu Chalres Boniface Mkwassa, sasa hivi sio tena kocha wa timu yetu ya taifa.
Taarifa hivi zimethibitishwa na rais wa TFF ndugu Jamal Malinzi kupitia ukurasa wa twitter. Jamal Malinzi ametoa taarifa hiyo kwa kuandika,“Mkataba wa TFF na Kocha Mkwassa,kwa makubaliano,umefikia mwisho leo.Salum Mayanga ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda wa Taifa Stars.”.

Ikumbukwe kamba kocha huyu alichukua mikoba kutoka kwa kocha Mart Nooij raia wa Uholanzi ambae alifundisha tangu mwaka 2014 hadi 2015.
TFF imemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda, wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kuchukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.
![]() |
Salum Mayanga |
Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.
0 comments:
POST A COMMENT