Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokana na "mzozo wa rasilimali", Tume ya Mahakama ya Uchunguzi iliyopewa kazi ya kuchunguza mauaji hayo ilihitimisha katika ripoti yake iliyowasilishwa kwa Raisi Uhuru Kenyatta Jumatano (tarehe 22 Mei).
Hakimu Bi. Grace Nzioka aliwasilisha ripoti kwa Kenyatta miezi saba
baada ya tarehe ya awali iliyokuwa itolewe mwezi Oktoba. Kenyatta
aliahidi kupitia mambo yaliyogunduliwa na tume na "kuchukua hatua
zinazofaa," kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya habari ya Raisi.
Matokeo yanaondoa shutuma za awali kwa Inspekta Mkuu wa Polisi David
Kimaiyo na wengine kwamba vurugu huko Mto Tana ilikuwa iliyochochewa na
wanasiasa.
Aliyekuwa Msaidizi wa Waziri Dhadho Godhana aliondolewa kutoka wadhifa wake baada ya kushutumiwa kuhusika katika mapambano hayo. Baadaye aliachiliwa na Mahakama Kuu.
0 comments:
POST A COMMENT