Kenyatta ataja mawaziri wawili wa mwisho Mei 23, 2013 | Gossip Wire
Breaking News
Loading...

Friday, May 24, 2013

Kenyatta ataja mawaziri wawili wa mwisho Mei 23, 2013

Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya baraza lake la mawaziri lenye wajumbe 18, mwezi mmoja tangu mchakato wa uteuzi kuanza.




Mei 23, 2013
Meneja wa hoteli ya Utalii Joseph Ole Lenku ameteuliwa kwa nafasi ya mambo ya ndani na uratibu wa serikali ya kitaifa, na mbunge wa zamani Samuel Kazungu Kambi kuwa waziri wa kazi, usalama wa jamii na huduma.
"Hatimaye nimeshapeleka majina bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa," Kenyatta alisema, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya.
Kamati ya bunge ya uteuzi itawachunguza wawili hao na kupeleka ripoti kwa Bunge la Taifa.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT