Gossip Wire

Gossip Wire

Breaking News
Loading...

Thursday, May 30, 2019

SEHEMU 4 za Mwili Usizopaswa Kumshika Mkeo Nyakati Hizi 18+..!!!


Ingawa kuna mtazamo uliojengeka katika jamii kuwa ukishamuoa mwanamke na mkawa mwili mmoja basi una kila haki ya kumshika sehemu yoyote uipendayo hasa wakati unahitaji kufanya nae tendo la ndoa.

Lakini utafiti na uzoefu uliokusanywa na wataalam wa mahusiano na ndoa waliofanya mahojiano na wanawake kama kuna sehemu wazisopenda kuguswa na waume zao na nyakati husika, umetoa picha na mtazamo ambao wanaume wanapaswa kuufahamu mapema kabla hawajaingia katika hatari ya kuwa kero au kuwakwaza wake zao.

Kama tunavyofahamu, wanawake ni viumbe wenya mlango mmoja wa ziada wa fahamu kuwapita wanaume. Hii nitaizungumzia siku nyingine. Lakini mlango huu wa ziada ndio huwapa hisia ya ziada pamoja na kuwafanya kujali sana vitu ambavyo mwanaume hasa mwenye haja ya kufanya tendo anaweza asizingatie sana anataka kukidhi haja yake.

Ukifuatilia sehemu hizi za mwili wa mwanamke nitakazozitaja na nyakati zake, utabaini kuwa ni rahisi sana kufahamu kwani mwanamke katika nyakati hizo anaweza kuonesha kusita sana wakati anataka kuguswa.

1. Chuchu wakati miili yao inaendelea na shughuli nyingine za ndani

Idadi kubwa ya wanawake huwa hawapendi kuguswa na wanaume chuchu zao wakati wananyonyesha au wakati wako katika hedhi. Hiki ni kipindi ambacho kama mwanamke ananyonyesha na mwanaume anataka kumgusa sehemu hiyo basi maziwa yanaweza kutoka kwa kasi na kumfanya ajisikie hayuko ‘confortable’ kuendelea na zoezi la kushiriki tendo.

2. Kwapani wanapokuwa wanatoka jasho kabla ya kuoga

Wanaume wengine huwa na hisia za matamanio zaidi wanapoyaona makwapa ya wake zao. Hii ni hali ya kisaikolojia inayojengeka kwa baadhi japo sio wengi. Kuna wanaume wakiona kwapa la mwanamke basi matamanio yao huongezeka mara dufu. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hujisikia vibaya na kukosa amani pale wanaume zao wanajaribu kuwashika kwapani wakati ambapo wametokwa jasho.

3. Sehemu za siri kabla ya kuoga

Hili ni eneo ambalo wanawake wengi wameonesha kulalamikia waume zao. Kwa mazoea wanaume wengi huwa kama wanawabaka wake zao bila kufahamu, hasa pale wanapotoka safari zao wakiwa na matamanio. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hupoteza hali ya kuwa ‘comfortable’ pale wanapoguswa na wanaume zao sehemu za siri wakati bado hawajaoga.

Wanaume wengi hujikuta wakishiriki tendo la ndoa na wake zao ghafla baada ya kukamilisha kazi kadhaa za ndani wakati wanawaangalia. Wanaume wanaweza kuwa wanafurahia zaidi tendo hilo lakini wanawake pamoja na kwamba hufurahia pia lakini mlango wao wa ziada wa fahamu huwafanya kukosa amani kwa kiasi fulani wakati wa tendo ukilinganisha na nyakati ambazo wanajiamini ni wasafi.

4. Nywele zao dakika chache baada ya kutoka saloon kujiremba

Ingawa unaamini kuwa mkeo alienda saloon kujiremba kwa ajili ya kukuvutia wewe, usithubutu kutaka kuzivuruga nywele zake dakika chache baada ya kutoka kwa mtaalam wa kutengeneza nywele, hata kama pesa aliyotumia ulimpa wewe.

Hiki ni kama kituko hivi, lakini ndio ukweli. Wanawake hutumia muda mrefu sana kwenye vibanda au saloon za gharama kwa ajili ya kujiremba ili waongeze mvuto. Lakini, hugeuka kuwa walinzi wa vichwa vyao angalau kwa saa kadhaa. Msifie uwezavyo, lakini nywele zake usizivuruge mapema mtaharibiana ‘mood’.

Haya ni kati ya mambo machache ambayo wanaume huyaona madogo sana na kufuatilia yale wanayoamini ni makubwa zaidi. Lakini mambo haya ni kati ya machache yanayokwangua taratibu kuta za hisia za mwanamke kwa mmewe

Tuesday, June 6, 2017

Ubuyu wa Moto Moto..Idris Sultan Afilisika Milioni 500 Alizoshinda Big Brother..Ashindwa Kulipia Kodi ya Ghorofa Alilokuwa Anaishi..!!!


Wapenda ubuyu wanakuambia hakuna kinachodumu milele duniani! Ndiyo maneno unayoweza kusema kutokana na maisha ya Mshindi wa Big Brother Africa (BBA) mwaka 2014, Idris Sultan ambayo anaishi kwa sasa.

Kwa mujibu wa watoa ubuyu, mai­sha ya jamaa huyo ni tofauti kabisa na matarajio ya wengi kutokana na mshiko aliovuta BBA wa zaidi shilingi milioni 500 za Kibongo.

NDIYO CHOKA MBAYA?

Inasemekana kuwa, ishu hiyo ndiyo ilizua maswali kwa watu wake wa karibu wakihoji ndiyo jamaa amekuwa choka mbaya? Vyanzo makini vilil­iambia Wikienda kuwa, kwa sasa Idris anaonekana amechoka mbaya kwani anadaiwa kuhama kwenye jumba la ghorofa alilokuwa akiishi Mbezi-Beach jijini Dar na kuhamia kwenye chumba kimoja maeneo ya Mbezi-Chini, Dar.

“Kiukweli maisha anayoishi Idris yanashangaza sana na inaonekana ameshamaliza zile shilingi milioni mia tano alizoshinda BBA.“

Inaonekana zimekata maana siyo wa kwenda kupanga chumba kimoja waka­ti mwanzoni kabisa baada ya kushinda alikuwa anaishi kwenye ghorofa na maisha yake yalikuwa ya mwendokasi (kufuru ya fedha) kwa kuwa mkwanja ulikuwepo.

“Kwa sasa anaishi maisha ya kawaida kama vile hajawahi kupata fedha nyingi kiasi kile. “Sasa sijui alizimalizia wapi fedha zote zile au aliendekeza sana bata maana vijana wengi wa Dar wanapenda kujiachia wanapopata fedha huku wakiendekeza tabia ya kubadilisha totozi kila kukicha,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa gazetini.

OFM WAMFUNGIA KAZI

Baada ya kupata ubuyu huo, kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilicho chini ya Global Publishers kilimfungia kazi Idris am­bapo walifika Mbezi-Chini anakodaiwa kuishi kwenye chumba kimoja.

MAJIRANI WAFUNGUKA

Walipofika anakoishi, OFM walijifanya wageni wake, lakini wapangaji wenzake walidai kuwa alitoka. Hata hivyo, jibu hilo liliwathibitishia OFM kuwa Idris anaishi pale ambapo walipata fursa ya kuoneshwa mlango cha chumba chake.Mazingira ambayo OFM ilishuhudia ni tofauti na maisha aliyokuwa akiishi awali ambapo ilibidi kufotoa picha kadhaa.“Ni kweli hapa ndipo anapoishi Idris kwa upande wa mbele wa nyumba hii lakini kwa sasa hayupo, naona ameenda kazini (kwa sasa ni Mtangaz­aji wa Choice FM na ni msanii wa vichekesho,” alisema jirani mmoja aliyeomba hifadhi ya jina ili asije akaonekana ‘mnoko’ na kutibua ujirani mwema na staa huyo na kuongeza:

“Lakini ni mtu mzuri na tunafurahi kuishi na staa.”

IDRIS ASAKWA

Baada ya kumkosa nyumbani hapo, OFM walimsaka Idris kwa njia ya simu lakini iliita bila kupokelewa.

Hata hivyo, baadaye ali­tuma ujumbe mfupi kwamba atumiwe meseji ambapo mazungumzo yalikuwa hivi;

OFM: Kuna habari kwamba kwa sasa ume­filisika na unaishi kwenye chumba kimoja, tofauti na mwanzo ulivyokuwa unaishi kwenye ghorofa la ukweli, hii ishu ikoje?

Idris: Haahaaa..! Hivi nina endorsements (mi­kataba ya madili) ngapi? Ukipiga hesabu ukakadiria utakuwa unajua nina thamani gani. Ila unaruhusiwa kuhisi vingine.

OFM: Sawa, lakini sisi ni vijumbe tu. Mashabiki wako wanataka uweke wazi kuhusu fedha ulizopata ziliishia wapi ili kumaliza maneno yanayozungumzwa?

Idris: Huwezi kuzuia watu kuzungumza ndugu yangu. Nikianza kuwaza mangapi ya kuyaweka wazi, nitajikuta ninajieleza kutwa kucha.

NENO LA MHARIRI

Sisi kazi yetu ni kumfikishia ubuyu mhusika na ndicho tulichokifanya lakini ni vizuri Idris akaweka mambo hayo wazi kwa sababu shilingi milioni 500 kukata kwenye mazin­gira kama hayo kunazua maswali mengi.

Masikini Johari wa Bongo Movies...Apata Pigo la Maisha


Pole! Staa wa kitambo wa sinema za Kibongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ amepata pigo ‘hevi’ baada ya kufiwa na shangazi yake aliyemlea tangu akiwa mtoto, kumsomesha na kumfundisha maisha hivyo kuondoka kwake kumemuachia maumivu na pigo kubwa.

Johari, akiwa nyumbani kwao mkoani Shinyanga kuhudhuria msiba huo aliliambia Wikienda kwa njia ya simu kuwa, aliumia mno alipopata taarifa za kifo cha shangazi yake huyo aliyekuwa nguzo muhimu maishani mwake.

“Nimekuja Shinyanga kumzika shangazi yangu, tumeshamzika, lakini kwa kweli ameniacha mpweke sana maana ndiye aliyenilea, kunisomesha na kunifundisha maisha, kiukweli ni pigo kwangu,” alisema Johari.

Thursday, May 18, 2017

UNDANI wa Kifo cha Dogo Mfaume na Ugonjwa Uliomuua...Uswahilini Simanzi tupu



DAR ES SALAAM: Rest In Peace Dogo! Haya ndiyo maneno tunayoweza kusema baada ya kupata taarifa za kushtusha za kifo cha msanii maarufu wa nyimbo za Mchiriku na Mnanda, Dogo Mfaume aliyefariki dunia jana mchana wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Amani lina data za kutosha. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Dogo Mfaume alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kichwani na kwamba kesho, alikuwa katika ratiba ya kufanyiwa upasuaji baada ya tatizo hilo kumsumbua kwa miezi kadhaa.

KUTOKA SOBER HOUSE, KIGAMBONI

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Pilli Missanah Foundation, Pilli Missanah, Dogo Mfaume ambaye kwa muda mrefu alikuwa katika kituo hicho akipatiwa matibabu ya kuachana na utumiaji wa madawa ya kulevya, alikimbizwa hospitalini baada ya afya yake kuzidi kuzorota. “Dogo Mfaume alikuwa na matatizo ya uvimbe kichwani kwa muda mrefu, ingawa pia alikuwa akisumbuliwa na magonjwa mengine kiasi kwamba alifikia wakati akashindwa hata kuongea. “Ugonjwa wake ulimsumbua kwa muda wa miezi mitatu, baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya tukalazimika kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi na kesho (Ijumaa) alikuwa afanyiwe upasuaji huo,” alisema Pili.



DOGO MFAUME NI NANI?

Wakati vijana wenzake wakitamba na Muziki wa Kizazi Kipya maarufu kama Bongo Fleva, Dogo Mfaume aliibuka katikati ya miaka ya 2000 akiimba muziki wa mitaani, ambao ulionekana kama wa kihuni zaidi, wa Mchiriku na
Mnanda, ambako alifanikiwa kujitengenezea jina kubwa baada ya nyimbo zake mbili, Hereni na Kazi yangu ya Dukani kumfikisha kileleni. Mwaka 2009 akiwa katika ubora wake, Dogo Mfaume alitwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Muziki Asilia kupitia kibao chake hicho cha Kazi Yangu ya Dukani.

INTERVIEW YA MWISHO NA GLOBAL TV

Miezi michache iliyopita, Dogo Mfaume alifanya mahojiano na Global TV Online, akiwa katika kituo cha kusaidia kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambapo alizungumza mambo mbalimbali kuhusiana na safari yake ya matumizi ya madawa ya
kulevya.


JINSI ALIVYOANZA ‘KULA UNGA’

“Mimi nilikuwa navuta bangi tu, sasa siku moja nilikuwa nimekwenda kujiweni nikamkuta mshkaji anavuta, nikamgongea nikijua ni bangi tu ya kawaida. Sasa yule jamaa hakutaka kuniambia ukweli, aliogopa pengine ninaweza kwenda kumtangazia kwa watu na asingeweza kuninyima maana nisingemwelewa. “Kwa hiyo akanipa, nikapiga pafu tatu akaninyang’anya, akavuta tena mara kadhaa akanipa, nikavuta tena, nilipomaliza, nikaona raha f’lani ambayo sijawahi kuiona tangu nianze kuvuta bangi. Nikaanza kama kusinzia hivi kitu ambacho siyo kawaida.”

ATOA UJUMBE MZITO

“Kusema kweli ile raha ilinifanya kesho yake nimtafute yule mshkaji nikamuuliza vipi ile kitu ya jana, akaniambia ili tuipate, inatakiwa buku (shilingi elfu moja) nikampa mia tano na yeye akatoa mia tano, akaenda kuchukua, tukavuta. “Hivyo ndivyo nilivyoanza kuvuta, hii kitu ukianza siyo rahisi kuacha, ndivyo hivyo ilivyokuwa.”

NIMETESEKA MIAKA SABA

“Nimetumia madawa ya kulevya kwa muda wa miaka saba, mwanzo nilikuwa najifichaficha watu wasinione, lakini hali ilivyozidi nikajikuta sioni aibu tena, badala ya kwenda kununuliwa nikawa naenda mwenyewe.”
Wakati mamia ya mashabiki wa Mchiriku nchini wakiamini kuwa Kibao cha Kazi Yangu ya Dukani, kilimpa mafanikio makubwa msanii huyo kimuziki na kimaisha, ukweli kutoka mdomoni mwake ni kuwa wimbo huo ndiyo ulichangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka na hatimaye kuharibika kabisa kwa maisha yake.


“Nilikuwa nimeshaanza kutumia unga wakati natoa kile Kibao cha Kazi Yangu ya Dukani, kusema ukweli wimbo ule ndiyo ulichangia sana kuniangamiza, kwa sababu nilikutana na watu wengi na pia nilipata pesa nyingi, nilikuwa sina mke, sina majukumu, kwa hiyo kadiri nilivyopata pesa ndiyo kasi ya kubwia ilivyozidi

“Kuna siku tulikuwa tumealikwa kwenye shoo sehemu, ilipofika zamu yangu nikaitwa kupanda jukwaani, sasa nilivyoshika mic tu, mtu mmoja aliyekuwa karibu akaanza kupayuka kwa sauti, toa teja hilooo, toa teja hilooo, tumetoa hela yetu hatutaki mateja sisi…Dah! Jamaa alinitoa kabisa kwenye reli, sitakisahau kile kitendo. “Nilimuona jamaa kama ndiyo ananitangazia kwa sababu wakati anasema, alikuwa akisikika katika spika, nikajua Tanzania nzima watajua kama nakula unga maana hadi wakati huo nilitam
bua kuwa hakuna mtu aliyekuwa anajua,” alisema Dogo Mfaume.

Hadi Amani linakwenda mitamboni kulikuwa hakuna taarifa zozote kutoka kwa familia yake, kuhusu msiba na shughuli za mazishi, lakini baadhi ya wasanii wenzake, kupitia mitandao ya kijamii, walizungumzia kifo hicho cha mmoja wa wasanii walioacha alama katika Mchiriku. Wasanii ambao walikuwa wameposti kuhusiana na msiba huo ni pamoja na Mr. Blue, Mheshimiwa Temba, Chegge Chigunda, Nay wa Mitego na Dulla Makabila walionesha kumlilia. Aidha, mitaani hasa uswahili ambako alikuwa na mashabiki wengi kufuatia aina ya muziki aliokuwa akifanya, simanzi imetawala hasa kufuatia taarifa kuwa, ilikuwa arejee kwenye game baada ya afya yake kutengemaa. Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu, Amina. Kwa habari kuhusiana na maisha ya Dogo Mfaume kabla ya kufikwa na mauti.

GPL

PICHA: Hospitali Marekani yafanikisha upasuaji mkubwa wa wanafunzi Walionusurika katika Ajali

Watoto watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vicent walionusurika katika ajali ya basi, wamefanyiwa upasuaji na sasa wapo wodini wakiendelea na mazoeazi, ila Doreen, jana alipewa MAPUMZIKO maalumu akiwa anaandaliwa tayari kwa UPASUAJI wa uti wa mgongo 'spine'  unaofanyika leo.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyeshiriki katika kuwasafirisha watoto hao, ameandika katika ukurasa wake wa facebook akisema  watoto hao kwa sasa wamewekwa kwenye vyumba vya peke yao.

 Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani.

 Amefafanua upasuaji waliofanyiwa na kusema mtoto Saidia alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa kulia wa nyonga, mkono wa kulia na kuwekewa ngao kwenye shingo atakayotakiwa kukaa nayo kwa wiki sita.

“Kwa upande wa mtoto Wilson, yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga ya kulia, kiwiko cha kulia kilichokuwa kimevunjika mara tatu na kiwiko cha kushoto,” amesema

Amesema Doreen yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga, taya katika upasuaji uliochukua saa nne. Leo Doreen atafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo. 

Monday, May 15, 2017

Gigy Amchefua Wema Ukumbini



Muuza nyago kwenye video za nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’anadaiwa kumtia hasira na kumchefua staa wa sineza za Kibongo, Wema Isaac Sepetubaada ya kukutana ukumbini kwenye bethidei ya meneja wa wasanii wa muziki.

Ubuyu wa motomoto ulidai kuwa, baada ya kukutana, Gigy alidaiwa kucheza muziki kihasarahasara na mmoja wa ‘mazilipendwa’ wa Wema, jambo ambalo mlimbwende huyo hakupendezwa nalo.

Ishu hiyo ilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel uliopo Posta jijini Dar ambapo mastaa kibao walikuwa wageni waalikwa kwenye shughuli hiyo iliyotawaliwa na mavazi ya kizamani.

Kwa mujibu wa shushushu waWikienda aliyekuwa ndani ya shughuli hiyo, awali Wema alionekana mwenye bashasha tele akiwa na wapambe wake, lakini Gigy alipoanza makeke yake ndipo bibie huyo akapoa kama maji ya mtungi.

“Mwanzoni Wema hakuwa na tatizo kabisa na Gigy, lakini baada ya mwanadada huyo kwenda kucheza kihasara na zilipendwa wa Madam (Wema) hapo ndipo balaa likaibuka, akanywea na kumkata jicho la hasira, hata wale wapambe wake (Wema) wakaanza kumvimbia Gigy baada ya kuona anataka kuharibu shangwe za mama la mama.

“Gigy alionekana ni mwenye furaha tele, kwani alikuwa amepiga maji ya kutosha (pombe) hivyo hakujali hata kidogo kama anamkwaza mtu, isitoshe kilichoharibu zaidi ni baada ya jamaa kunogewa na manjonjo ya Gigy na kumzawadia wigi lake alilokuwa amevaa,” aliongeza sosi.

Baada ya kuinyaka ishu hiyo,Wikienda lilimtafuta Gigy na kumuuliza kulikoni kumkera Wema kwa kumchezea vibaya bwana wake wa zamani ambapo bila hiyana alifunguka:

“Ni kweli nilicheza na huyo mtu tena kwa kujinafasi kwa sababu ilikuwa ni sehemu ya furaha, sikuona sababu ya kujivunga eti kwa sababu nitamuudhi Wema au mtu yeyote yule.

“Kwanza yeye ameshaachana naye kitambo kama bado ana wivu naye atajijua mwenyewe,” alisema Gigy.

Jitihada za kumpata Wema hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa chatting kupitia WhatsApp zilionesha kupokelewa lakini hakujibu.

Imeandikwa na Mayasa Mariwata na Gladness Mallya

Thursday, May 11, 2017

Mambo 7 yanayowaumiza wanaume kwenye mahusiano



Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au kuachwa.

Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake.

Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine, ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu. Hajui chanzo cha yeye
kukimbiwa.

Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda. Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau na yeye aitwe mama.

Wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenzi wao kwa sababu ya tabia fulani ambazo wakati mwingine huanza taratibu na baadaye huwa kikwazo kikubwa.

Ili kuweza kuepukana na tatizo hili ni vyema tukaangalia vitu ambavyo wanaume wamekuwa hawavipendi kutoka kwa wanawake ili kuweza kujua nini cha kufanya kuhakikisha unamweka mwanaume karibu, asikuache.

1. Chokochoko/Maneno Maneno 
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.

Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.

2. Kutoridhika
Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.
Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.

Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.

Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake hamtimizii.

Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.

3. Kulinganisha
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’
Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.

Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.

Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.

4. Kuwa Tegemezi
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.
Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.

Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.

Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.

5. Kutokuwa Muelewa 
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.
Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.

6. Kujigamba/Maringo 
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.

Isikupite hii: Mambo matano '5' yatakayo kuongezea thamani katika maisha yako

Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.

7. Kuwa bize sana 
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.

Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.

MKAPA:Kwanini sikufanya uhakiki wa vyeti feki nilipokuwa madarakani



BAADA ya Rais John Magufuli Kubaini watumishi wenye vyeti feki kwenye Serikali na kuwatoa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjami Mkapa amejialumu kwanini hakuafkilia kuhakikia vyeti feki kwa watumishi wa umma alipokuwa madarakani

“Masikitiko yangu pekee ni kwamba kwa nini sikufanya uhakiki huu wakati nikiwa madarakani. Labda nilikuwa na mambo mengine makubwa zaidi niliyotakiwa kuyafanya lakini kwa hili alilofanya Magufuli namuunga mkono kabisa,” alisema Mkapa.

Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akifanya mahojiano na Shirika la Habari la Ujerumani (DW)  na Kumpongeza rais Magufuli  kwa kufanikisha zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti vya kughushi vya taaluma na kazi, na akasema anasikitika tu kwamba kwa nini yeye hakufanya hivyo wakati wa utawala wake.

''Wenye vyeti feki au watumishi hewa walikuwa wakiingizia serikali hasara wengine wakiendelea kukaa kazini bila ya kustaafu, hivyo lilikuwa ni jambo la lazima kufanyika ni kwa manufaa ya taifa" amesema


Kauli hii ya Rais Mkapa imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt Magufuli kuwaamuru watumishi wa umma 9,932 waondoke kwenye utumishi wao baada ya kubainika kughushi vyati vyao.

Wednesday, May 10, 2017

Job Ndugai Atembelewa Na Wabunge Wa Bunge La Umoja Wa Ulaya


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wanne kulia) akipiga picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Mhe. David Martin (wanne kushoto) baada ya kumalizika kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo pale alipopata ugeni wa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, katika Kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.



Wageni wa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ambao ni Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wakifwatilia Vikao vya Bunge vinavyoendelea leo Mjini Dodoma.

MSAADA..Nimedata na Manjonjo ya Huyu Changudoa Hadi Nafikiria Kumuacha Mke Wangu..!!!



Nikiwa katika pitapita zangu, nilimuona mtoto Mmoja mrembo Sana akiwa ameket kibarazani(Kama mita 500 kutoka ninapoishi)

Nilishangaa kuona navutiwa naye Sana kiasi cha kutotaka atoke machoni kwang, nilisogea Na kumpa hi, Aliitikia kwa sauti ya uchovu Sana (kimahaba)

Nilipiga naye story za hapa Na pale nikijidai natafuta chumba cha kupanga mitaa Ile, nikafanikiwa kupata namba yake ya simu..!

Mara kwa Mara nimekuwa nikicjat naye mida ya mchana maana alidai ameolewa, pia Na mm nna mke..!

Niliendelea kumchimba Ili kujua Maisha yake kiundani, ndipo nilipogundua kuwa anaish mjin kwa kuuza uchi wake...( Kuna meng Sana ya kuandika kuhusu suala hili ila ngoja niishie hapo kwani sio lengo)

Siku zilizid songa huku tukiendelea kuchati.Alianza kunitext usiku, nilichat naye huku nukiavoid hali hiyo maana mke akijua n tatizo, 

Ilifikia kpnd akawa anantumia picha zake za nusu uchi,akiwa na chupi,bikini na wakat mwngne alijiselfisha akiwa kifua wazi,( nilidata na maumbile ya huyu changudoa, chuchu zake zilisimama barabara)

Kidume nilikosa cha kufanya maana huyu dada alikuwa ananipeleka mbali Sana kihisia.., baada ya kuhakikisha mazingira ya kiusalama wa kiafya ya huyu dada ilinibidi nifanyenaye mapenziTu hakukuwa na namna..!

Kilichonileta hum Ni suala moja Tu, huyu dada anajua mapenz balaa kumzid wife maana nnakoelekea sifurahii penz la mke wangu, sasa najiuliza haya maujuzi mke wangu atayajuaje Ili niweze kufrah naye, na kunavitu nikisema nimuelekeze Ili nienjoy atastukia na kujiuliza nimeyajuaje..!

Niko njia panda wakuu, naomben ushaur maana mke Wang nampenda lakini huyu changudoa ananteka na maujuzi yakee..

Nifanyeje???!!!!

Je Diva Anamjibu Dkt. Mwakyembe Kuhusu Kupinga Wasanii Wasiimbe Nyimbo za Kisiasa?


Ni muda mchache baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kusema wasanii waachane na tabia ya kuimba nyimbo za kisiasa kwani hakuna msanii aliyewahi kufikia mafanikio makubwa kwa kufanya hivyo.


Mtangazaji Diva the Bawse kupitia mtandao wake wa twitter ameandika ujumbe ambao unasadikika pengine amejibu kauli ya waziri huyo.

Chid Benz Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kutoka Rehab ‘Stay Away From Drugs


Rapa Chid Benz amefunguka kwa mara ya kwanza tangia atoke Rehab alikokuwa akipata matibabu ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na amewaasa vijana watu,iaji wa Tanzania kuacha kabisa mchezo huo.

Chid Benz ambaye anaonekana mwenye afya na uso wenye furaha, amesema madawa ya kulevya sio ya kuyazungumzia. Amesema kama mtu hataki kujutia maisha yake yote basi aachane na mchezo huo mara moja.


“Stay away from Drugs,wakae mbali sana na madawa ya kulevya kitu kibaya sana sitaki kuongelea sana lakini wajitahidi (Watanzania) kadri wanavyoweza wakae mbali na madawa ya kulevya ni kitu kibaya sana kinaweza kukufanya ujutie maisha yako yote“Alisema Chid Benz kwenye mahojiano yake na Muungwana

Saturday, May 6, 2017

FAIDA ya Kuvaa Socks Miguuni Wakati wa Tendo la Ndoa..!!!


Utafiti uliofanywa na jopo la watafiti wenye utaalam wa masuala ya uhusiano na saikolojia wa Chuo kikuu cha Wageningen nchini Uholanzi umebaini faida za kushiriki tendo la ndoa ukiwa umevaa socks miguuni.

Bila shaka utakuwa umewahi kuona picha za watu wanaotengeneza taswira ya wanandoa wakiwa kitandani na socks miguuni. Huenda waliuamini utafiti huu na baada ya kujaribu wakaona unazaa matunda wayatakayo.

Katika utafiti huo, waligundua kuwa uvaaji wa socks miguuni kwa wanaume na wanawake kunaongeza ari zaidi na uwezekano wa kufika kileleni kwa haraka na mshindo wa nguvu zaidi kutoka 50% (kabla ya kuvaa socks) na 80% (baada ya kuvaa socksi).

Utafiti huo ulizaliwa kutoka kwenye ule wa awali ulifanywa mwaka 2011 na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Watafiti wa Johns Hopikins walikuwa wakijaribu kuusoma ubongo wa binadamu wakati akishiriki tendo la ndoa, kujua madhara ya kisaikolojia na kimwili anayoyapata wakati anapofika kileleni.

Wakati wakiendelea na na zoezi hilo, watu waliokuwa wanatumika kama sampuli wakifanya mapenzi, walilalamikia hali ya ubaridi ndani ya chumba chenye ‘scanner’ ya ubongo. Ndipo watafiti hao walipoamua kuwavalisha socks miguuni. Ghafla uwezo wao katika tendo hilo ulipanda kutoka 50% hadi 80% za kukifikia kilele kwa kishindo zaidi.

Nao watafiti wa Chuo Kikuu cha Wageningen wamebaini kuwa kuiweka miguu pekee kwenye hali ya joto kupitia socks, kunaongeza kwa asilimia za za ziada 30.

Sababu za kwanini Wanandoa wengi hufanana




Ni miongoni mwa swali wanalojiuliza watu wengi kwanini Wanandoa wengi hufanana? sasa leo nimekuletea majibu ambapo Wanasayansi wa chuo kikuu Boston Marekani wamefanya uchunguzi na kugundua sababu kubwa ya wanandoa kufanana ni kuoa watu wanaoshea historia ya undugu mfano watu wa kabila moja.

Rapa Dj khalid na mke wake Nicole Tuck

Wanasayansi hao wamesema kitendo cha watu kwenda kuoa au kuolewa kwenye miji au vijiji walikotokea kuna changia Wanandoa wengi kujikuta wana sura zinazofanana kutokana na makabila mengi kuwa na sifa moja inayofanana mfano pua nyembaba, pua kubwa, macho madogo n.k

Sababu nyingine waliyoitoa ya kwanini Wanandoa wengine sio kabila moja lakini bado wanafanana, wanasema kwa kawaida ubongo wa binadamu huwa na hali ya kumuamini mtu ambaye anavitu vinavyoendana na yeye na hali hii hupelekea watu kuoa au kuolewa na watu wanaofana vitu.

Staa wa 50 shades of grey Benedict Cumberbatch na Mke wake

Akielezea sababu ya kwanini wanandoa ambao walikua hawafanani hapo kabla kuanza kufanana baada ya miaka mingi kwenye ndoa, Mwanasaikolojia Robert Zajonc alisema jinsi wanandoa wanavyoishi inapelekea kufanana mfano Mwanaume anaye kasirika sana hutengeza mikunjo kwenye uso wake na Mwanaume wa aina hii humkasirisha mke wake pia ambaye naye atatengeza mikunjo ya uso hivyo kujikuta wamefanana.