Na Faraja Simon
Tuwe makini na wanasiasa na
tusiwaamini hata chembe hasahasa kwa hili la wao Kuhodhi mchakato wa uandishi
wa katiba mpya.
Siasa ni sehemu ya maisha ya kila
mtanzania hatuwezi kujitenga na siasa au siasa kutengwa nasi kwani imebeba
mustakabali wa taifa letu.Pamoja na kuwa katiba ni political document , tuwe
makini na siasa kuhodhi mchakato mzima wa bunge la katiba.Tusiruhusu wanasiasa
kutufanyia maamuzi kwa madai kwamba ndio maamuzi ya watanzania zaidi ya milioni
44.Sio Madai na hoja zote za wanasiasa ni madai ya wananchi.N sio kweli kwamba
wengi wao watasimamia na kutetea hoja za wananchi.
Wanasiasa watatafuta afueni ya
vyama vyao hapo badae.Watawala wanatafuta katiba itakayotoa mwanya wa wao
kuendelea kushika dola na wapinzania wanataka katiba itakayo wapa mwanya wa wao
kushika dola kirahisi.Wanasiasa watatetea ugali wa watoto wao na nafasi zao
hapo badae. Wengine wanatafuta ahuheni ya nafasi zao na za makundi yao hapo
baadaye.Kwa hivyo ni wachache sana wanaofanya maamuzi yao kitaifa pasi na
chembe za uchama.
Tusisahau kuwa uzalendo kwa
wanasiasa wetu si wa kuridhisha, namaanisha ubinafsi umetawala fikra zaoWengi
wao ni wachumia tumbo ,tusipokuwa makini watatuharibia katiba yetu kwa kuandika
katiba yenye misingi na matakwa yao.Pamoja na kwamba tuna nafasi ya kuipigia
kura ila tusisahau wanasiasa wana sauti ya kuwaaminisha watanzania visivyo vya
kweli na kwa kuwaamini, tukawafuata.Hii itakuwa hatari kubwa kwa taifa letu.
Hatuna budi kuijenga,kuilinda na
kuitetea Tanzania tunayoitaka. Ni Tanzania thabiti na yenye nguvu kubwa
kiuchumi, kiusalama, siasa safi zenye lengo la kumkomboa mwananchi pale tu
uzalendo utakapotunzwa kama lulu katika mioyo ya watanzania, pale rushwa
atakapokuwa adui wa kila mtanzania, na Pale viongozi wa taifa hili watakapozika
ubinafsi na kuishi uzalendo, kutetea rasilimali za taifa kwa manufaa ya taifa
hili, wakiongoza mgawanyo sawa wa matunda ya rasilimali kwa taifa.
Tanzania inahitaji mabadiliko
katika Nyanja zote.Hatuwezi kukataa mabadiliko au kuyapinga, tutayachelewesha
tu.Tanzania inahitaji viongozi watendaji na sio waongeaji,watakaothubutu kuwa
chachu ya mabadiliko chanya katika nyanja zote za maisha ya Mtanzania. Viongozi
wenye maamuzi ya kizalendo kwa manufaa ya watanzania.Maamuzi wanayoyafanya au
waliyowahi kuyafanya viongozi wetu kwa maslahi yao binafsi au ya mrengo wao
yamelitafuna taifa na kuliweka hapa lilipo, yamepoteza dira ya Tanzania kama
taifa.
Naamini Tanzania tunayoitaka ipo
na itakuwa.Vijana tunaweza kuweka pembeni itikadi za kisiasa na kidini,
ukabila, na ubinafsi.Na kuuvaa uzalendo na spirit ya kufanya kazi kwa
bidii,kuichukia rushwa kwa moyo wetu wote,
kuwa watendaji zaidi ya waongeaji kwa manufaa ya Tanzania yetu. Tusiseme
"walikula sasa zamu yetu".Bali tupatapo nafasi twende tukafanye kazi
ya kuwatumikia watanzania kwa uaminifu na uzalendo wa hali ya juu.Tuwe na fikra
za mabadiliko kwani naamini ipo siku vijana tutaandika historia mpya kwa taifa
hili.
Na Faraja simon
0 comments:
POST A COMMENT