Mwalimu Julius K Nyerere |
Na Faraja Simon
Uchaguzi wa mwaka mkuu umekaribi, bali
tutaanza na uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa.Nimejaribu kufikiri dhana pana
ya uongozi katika taifa hili.Nimefikiri juu ya utayari wa viongozi wetu kutatua
matatizo tuliyonayo kama wananchi, si utayari tu pia na uwezo wao katika katika
dhana ya uwajibikaji.
Wengi wa viongozi wetu wapo tayari waongoze
mpaka wanakufa, wanasahau kuwa uongozi ni dhamana anapewa na wananchi kwa muda
maalum. Anasahau kuwa kuna wengine wenye uwezo wa kushika nafasi hizo na kuleta
fikra mpya na mabadiliko kuendana na uhitaji wa taifa na wananchi kwa ujumla
wake. Wako tayari kuibaka demokrasia ili wabaki madarakani kwa kutumia esa kama
silaha ya kuendelea kutawala.Hili nimeliona sana kwa wabunge na madiwani.Nikaona
si vibaya tukijikumbusha maneno haya ya mwalimu nyerere. Aliyoyasema ni dhahiri
kuwa yanatokea sasa. Mwalimu alisema:
"Plato, myunani wa kale, alipendekeza kuwa mafilosofa ndio wanaofaa kuwa watawala wa nchi, maana wana sifa mbili muhimu: Kwanza wana uwezo wa kutawala, na pili hawapendi kutawala. kwa hiyo jamhuri ya plato itakuwa na sheria ya kuwalazimisha mafilosofa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikiisha, atafurahi sana kurudia shughuli zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazozipenda. lakini nchi zetu hazitawaliwi na mafilosofa wa plato; Watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala, hata kama hawana uwezo wa kutawala; na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa watawala, na wakisha kuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. " (uongozi wetu na hatima ya tanzania. zimbabwe publishing house, 1993: 8)
Toa maoni yako juu ya maneno haya ya mwalimu
na mzalendo wa taifa letu.
0 comments:
POST A COMMENT