Gossip Wire: MAKALA
Breaking News
Loading...
Showing posts with label MAKALA. Show all posts
Showing posts with label MAKALA. Show all posts

Tuesday, May 6, 2014

WARAKA WANGU KWA VIJANA WENZANGU KWA MWAKA 2014: MAISHA BORA YANAJENGWA NA WEWE M WENYEWE UKIAMUA.



Na. FARAJA SIMON
Maadamu tupo hai tunanafasi ya kuboresha maisha yetu. Tusiache kutumia fursa tulizonazo hata kama ni ndogo, kuboresha maisha yetu. Kila mtu ana matatizo na vizuizi vingi katia safari ya kuhakikisha tunakuwa na maisha bora.Ukweli ni kwamba hayo yote hayatufanyi kutofikia ndoto zetu.Matatizo yasitukatishe tamaa bali tuyachukulie kama changamoto katika kuboresha maisha yetu kisha tusonge mbele na kamwe tusirudi nyuma.

Bidii ya kazi ni muhimu sana,tuwe na moyo mkuu katika kufanya kazi kwa bidii huku tukijiwekea malengo mafupi na marefu kadiri muda utakavyoruhusu.Tusisahau muda si mali yetu,hivyo tusisubiri kesho wala badae ikiwa mungu katupa uzima.Tufanye kazi bila kudharau kazi kwani hakuna aliyeanza na mamilioni bali wote wameanzia chini.

Tuondoe  fikra kwamba kazi hii si hadhi yangu au ile ni hadhi yangu.Kazi haina hadhi ilimradi inaingiza kipato hata kama ni kidogo kwani si sawa na kukaa bure.Upatapo fursa ya kufuga kuku itumie na ipende nayo itakutoa.ikiwa umepata fursa ya kulima basi itumie ipasavyo na bila kukata tamaa, utayaona mafanikio.Sio lazima sote tukae katika ofisi zenye viyoyozi ndo ujione kuwa una kazi. Kijana kazana na chochote unachoweza kukifanya, usikate tamaa, chukua hatua nyingine mbele uweze kufikia lengo lako.

Ni vyema kutafuta elimu ya ujasiriamali ili tuweze kutawala fedha vyema na kutengeneza michanganuo ya biashara kwa ustadi mkubwa. Pia kufanya tafiti kwa waliopiga hatua kiuchumi. Hii itatusaidia kwenda na kasi ya dunia ya sasa.Pia itatufungua zaidi juu ya kuzitambua fursa zinazotunguka. Hii itaongeza ujasiri wa kuthubutu kwetu sisi vijana.Safari si ndefu sana, Reginald Mengi (kwa mfano) tutamfikia tu kwani hakuanza juu bali alianza chini kwenda juu.Vijana wenzangu wa kitanzania Tusikate tamaa kesho yetu imekwisha kufika.

Serikali bora, sikivu na mathubuti ni moja ya chachu muhimu katika maendeleo ya vijana.hivyo, shime, shime vijana tupatapo nafasi ya kufanya uchaguzi tuitumie kwa busara na hekima zilizotukuka kuchagua viongozi watakaotufungulia fursa za kuiona kesho yetu.Viongozi watakaoona ipo sababu ya kuwalinda vijana na kuwaongoza katika kujikwamua kiuchumi.tusichague kiongozi kwa sababu ya ushabiki wa kichama, kikanda, kikabila, kidini, kindugu wala kwa kufata mkumbo.baada ya kusikiliza sera zao  ni vyema tukafanya uchanganuzi binafsi na maamuzi binafsi juu ya mustakabali wa taifa letu na maisha yetu kwa kuchagua kiongozi bora na atakayetuongoza katika kuipeleka nchi yetu mahala bora zaidi.

Vijana wenzangu, Maisha bora yanajengwa na wewe mwenyewe ukiamua.Maisha bora yanaanzia kwako kwako.Weka nia, bidii, na jitihada za dhati pamoja na ujasiri wa kuthubutu katika kujijenga kiuchumi tutumie fursa zilizopo tukiuheshimu muda nasi tutaboresha maisha yetu.Kijana chukua hatua madhubuti kuweza kujikwamua kiuchumi.
 Imeandikwa na Faraja Simon
            Email: farajasimon@yahoo.comfarajasimonm@gmail.com
            mobile: +255787539392, +255763222443

Tuesday, March 25, 2014

NIMEONA LEO TUTAFAKARI MANENO HAYA YA MWALIMU YANAYOISHI.

Mwalimu Julius K Nyerere



Na Faraja Simon
Uchaguzi wa mwaka mkuu umekaribi, bali tutaanza na uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa.Nimejaribu kufikiri dhana pana ya uongozi katika taifa hili.Nimefikiri juu ya utayari wa viongozi wetu kutatua matatizo tuliyonayo kama wananchi, si utayari tu pia na uwezo wao katika katika dhana ya uwajibikaji.
Wengi wa viongozi wetu wapo tayari waongoze mpaka wanakufa, wanasahau kuwa uongozi ni dhamana anapewa na wananchi kwa muda maalum. Anasahau kuwa kuna wengine wenye uwezo wa kushika nafasi hizo na kuleta fikra mpya na mabadiliko kuendana na uhitaji wa taifa na wananchi kwa ujumla wake. Wako tayari kuibaka demokrasia ili wabaki madarakani kwa kutumia esa kama silaha ya kuendelea kutawala.Hili nimeliona sana kwa wabunge na madiwani.Nikaona si vibaya tukijikumbusha maneno haya ya mwalimu nyerere. Aliyoyasema ni dhahiri kuwa yanatokea sasa. Mwalimu alisema:


"Plato, myunani wa kale, alipendekeza kuwa mafilosofa ndio wanaofaa kuwa watawala wa nchi, maana wana sifa mbili muhimu: Kwanza wana uwezo wa kutawala, na pili hawapendi kutawala. kwa hiyo jamhuri ya plato itakuwa na sheria ya kuwalazimisha mafilosofa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikiisha, atafurahi sana kurudia shughuli zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazozipenda. lakini nchi zetu hazitawaliwi na mafilosofa wa plato; Watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala, hata kama hawana uwezo wa kutawala; na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa watawala, na wakisha kuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. " (uongozi wetu na hatima ya tanzania. zimbabwe publishing house, 1993: 8)


Toa maoni yako juu ya maneno haya ya mwalimu na mzalendo wa taifa letu.

TANZANIA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA



Na Faraja Simon
Tuwe makini na wanasiasa na tusiwaamini hata chembe hasahasa kwa hili la wao Kuhodhi mchakato wa uandishi wa katiba mpya.

Siasa ni sehemu ya maisha ya kila mtanzania hatuwezi kujitenga na siasa au siasa kutengwa nasi kwani imebeba mustakabali wa taifa letu.Pamoja na kuwa katiba ni political document , tuwe makini na siasa kuhodhi mchakato mzima wa bunge la katiba.Tusiruhusu wanasiasa kutufanyia maamuzi kwa madai kwamba ndio maamuzi ya watanzania zaidi ya milioni 44.Sio Madai na hoja zote za wanasiasa ni madai ya wananchi.N sio kweli kwamba wengi wao watasimamia na kutetea hoja za wananchi.

Wanasiasa watatafuta afueni ya vyama vyao hapo badae.Watawala wanatafuta katiba itakayotoa mwanya wa wao kuendelea kushika dola na wapinzania wanataka katiba itakayo wapa mwanya wa wao kushika dola kirahisi.Wanasiasa watatetea ugali wa watoto wao na nafasi zao hapo badae. Wengine wanatafuta ahuheni ya nafasi zao na za makundi yao hapo baadaye.Kwa hivyo ni wachache sana wanaofanya maamuzi yao kitaifa pasi na chembe za uchama.

Tusisahau kuwa uzalendo kwa wanasiasa wetu si wa kuridhisha, namaanisha ubinafsi umetawala fikra zaoWengi wao ni wachumia tumbo ,tusipokuwa makini watatuharibia katiba yetu kwa kuandika katiba yenye misingi na matakwa yao.Pamoja na kwamba tuna nafasi ya kuipigia kura ila tusisahau wanasiasa wana sauti ya kuwaaminisha watanzania visivyo vya kweli na kwa kuwaamini, tukawafuata.Hii itakuwa hatari kubwa kwa taifa letu.


Hatuna budi kuijenga,kuilinda na kuitetea Tanzania tunayoitaka. Ni Tanzania thabiti na yenye nguvu kubwa kiuchumi, kiusalama, siasa safi zenye lengo la kumkomboa mwananchi pale tu uzalendo utakapotunzwa kama lulu katika mioyo ya watanzania, pale rushwa atakapokuwa adui wa kila mtanzania, na Pale viongozi wa taifa hili watakapozika ubinafsi na kuishi uzalendo, kutetea rasilimali za taifa kwa manufaa ya taifa hili, wakiongoza mgawanyo sawa wa matunda ya rasilimali kwa taifa.


Tanzania inahitaji mabadiliko katika Nyanja zote.Hatuwezi kukataa mabadiliko au kuyapinga, tutayachelewesha tu.Tanzania inahitaji viongozi watendaji na sio waongeaji,watakaothubutu kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika nyanja zote za maisha ya Mtanzania. Viongozi wenye maamuzi ya kizalendo kwa manufaa ya watanzania.Maamuzi wanayoyafanya au waliyowahi kuyafanya viongozi wetu kwa maslahi yao binafsi au ya mrengo wao yamelitafuna taifa na kuliweka hapa lilipo, yamepoteza dira ya Tanzania kama taifa.


Naamini Tanzania tunayoitaka ipo na itakuwa.Vijana tunaweza kuweka pembeni itikadi za kisiasa na kidini, ukabila, na ubinafsi.Na kuuvaa uzalendo na spirit ya kufanya kazi kwa bidii,kuichukia rushwa kwa moyo wetu wote,  kuwa watendaji zaidi ya waongeaji kwa manufaa ya Tanzania yetu. Tusiseme "walikula sasa zamu yetu".Bali tupatapo nafasi twende tukafanye kazi ya kuwatumikia watanzania kwa uaminifu na uzalendo wa hali ya juu.Tuwe na fikra za mabadiliko kwani naamini ipo siku vijana tutaandika historia mpya kwa taifa hili.


Na Faraja simon