WARAKA WANGU KWA VIJANA WENZANGU KWA MWAKA 2014: MAISHA BORA YANAJENGWA NA WEWE M WENYEWE UKIAMUA. | Gossip Wire
Breaking News
Loading...

Tuesday, May 6, 2014

WARAKA WANGU KWA VIJANA WENZANGU KWA MWAKA 2014: MAISHA BORA YANAJENGWA NA WEWE M WENYEWE UKIAMUA.



Na. FARAJA SIMON
Maadamu tupo hai tunanafasi ya kuboresha maisha yetu. Tusiache kutumia fursa tulizonazo hata kama ni ndogo, kuboresha maisha yetu. Kila mtu ana matatizo na vizuizi vingi katia safari ya kuhakikisha tunakuwa na maisha bora.Ukweli ni kwamba hayo yote hayatufanyi kutofikia ndoto zetu.Matatizo yasitukatishe tamaa bali tuyachukulie kama changamoto katika kuboresha maisha yetu kisha tusonge mbele na kamwe tusirudi nyuma.

Bidii ya kazi ni muhimu sana,tuwe na moyo mkuu katika kufanya kazi kwa bidii huku tukijiwekea malengo mafupi na marefu kadiri muda utakavyoruhusu.Tusisahau muda si mali yetu,hivyo tusisubiri kesho wala badae ikiwa mungu katupa uzima.Tufanye kazi bila kudharau kazi kwani hakuna aliyeanza na mamilioni bali wote wameanzia chini.

Tuondoe  fikra kwamba kazi hii si hadhi yangu au ile ni hadhi yangu.Kazi haina hadhi ilimradi inaingiza kipato hata kama ni kidogo kwani si sawa na kukaa bure.Upatapo fursa ya kufuga kuku itumie na ipende nayo itakutoa.ikiwa umepata fursa ya kulima basi itumie ipasavyo na bila kukata tamaa, utayaona mafanikio.Sio lazima sote tukae katika ofisi zenye viyoyozi ndo ujione kuwa una kazi. Kijana kazana na chochote unachoweza kukifanya, usikate tamaa, chukua hatua nyingine mbele uweze kufikia lengo lako.

Ni vyema kutafuta elimu ya ujasiriamali ili tuweze kutawala fedha vyema na kutengeneza michanganuo ya biashara kwa ustadi mkubwa. Pia kufanya tafiti kwa waliopiga hatua kiuchumi. Hii itatusaidia kwenda na kasi ya dunia ya sasa.Pia itatufungua zaidi juu ya kuzitambua fursa zinazotunguka. Hii itaongeza ujasiri wa kuthubutu kwetu sisi vijana.Safari si ndefu sana, Reginald Mengi (kwa mfano) tutamfikia tu kwani hakuanza juu bali alianza chini kwenda juu.Vijana wenzangu wa kitanzania Tusikate tamaa kesho yetu imekwisha kufika.

Serikali bora, sikivu na mathubuti ni moja ya chachu muhimu katika maendeleo ya vijana.hivyo, shime, shime vijana tupatapo nafasi ya kufanya uchaguzi tuitumie kwa busara na hekima zilizotukuka kuchagua viongozi watakaotufungulia fursa za kuiona kesho yetu.Viongozi watakaoona ipo sababu ya kuwalinda vijana na kuwaongoza katika kujikwamua kiuchumi.tusichague kiongozi kwa sababu ya ushabiki wa kichama, kikanda, kikabila, kidini, kindugu wala kwa kufata mkumbo.baada ya kusikiliza sera zao  ni vyema tukafanya uchanganuzi binafsi na maamuzi binafsi juu ya mustakabali wa taifa letu na maisha yetu kwa kuchagua kiongozi bora na atakayetuongoza katika kuipeleka nchi yetu mahala bora zaidi.

Vijana wenzangu, Maisha bora yanajengwa na wewe mwenyewe ukiamua.Maisha bora yanaanzia kwako kwako.Weka nia, bidii, na jitihada za dhati pamoja na ujasiri wa kuthubutu katika kujijenga kiuchumi tutumie fursa zilizopo tukiuheshimu muda nasi tutaboresha maisha yetu.Kijana chukua hatua madhubuti kuweza kujikwamua kiuchumi.
 Imeandikwa na Faraja Simon
            Email: farajasimon@yahoo.comfarajasimonm@gmail.com
            mobile: +255787539392, +255763222443

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT